Leo Inapenda kuwajuza ni Jinsi Gani unaweza Ku-update Au Kuongeza ububwa wa Android Version Ya Simu yako kwa kutumia ROM Husika kulingana na Kampuni Husika Simu.
Kati hali ya usalama ni wazi kuwa watu wengi sana wanatabia za kushika simu za watu bila kupewa ruhusa. Tabia hii ni kubwa sana miongoni mwetu kiasi kwamba leo imebidi kuja na makala hii ya jinsi ya kujua mtu anaeshika simu yako bila wewe kujua. Mbali na hayo njia hii pia inaweza kuwa msaada mkubwa pale unapopoteza simu yako kwani itakusaidia utaweza kujua aliyechukua simu yako moja kwa moja.
MAHITAJI
Bando la internet 80 MBSimu Husika Ya Android Account Ya EmailANGALIZO
Software Support Tanzania Hatutohusika kwa Uchochozi/Ugombanishi wala madhara yoyote yatakayo tokea kutokana na makala hii.
HATUA
1. Ingia kwenye Play Store kisha download App inayoitwa Intruder Selfie, unaweza kupata app hiyo kwa kutumia link hapo chini na utapelekwa kwenye Play Store kwaajili ya kudownload App hiyo.
2. Install vizuri kwenye simu yako unachotakiwa sasa ni kufungua app hiyo kisha fuatisha maelezo yote hapo chini.
3. Bonyeza sehemu ya Grant Permision kisha bofya OK kwenye kila permision ambayo application hii inahitaji, hatua hii ni muhimu ili kufanya app hii iweze kufanya kazi vizuri.
4. Bonyeza sehemu hii ya Grant Device Admin kisha bofya Acivate kwenye simu yako, sehemu hii ni muhimu sana kwani inasaidia mtu asiweze kuondoa app hii kwenye simu yako hadi pale utakapo taka wewe mwenyewe. Pia usisahau kuweka tiki kwenye kichumba kilicho andikwa I understand.
5. Bonyeza kwenye Activate
6. Ingia kwa kutumia akaunti yako ya Google, Hatua hii ni muhimu sana kama unataka kutumia app hii pale simu yako inapo potea au kuibiwa, Sehemu hii itakusaidia kuweza kupata picha ya mtu aliyechukua simu yako moja kwa moja na utaweza kuipata kupitia Google Photo.
7. Baada ya kufanikiwa kuingia kwenye app hiyo sasa utaweza kuona Menu yenye vimikato vitatu juu upande wa kushoto bofya hapo kisha bofya sehemu ya Settings.
8. Baada ya kubofya Setting utapelekwa kwenye uwanja wenye mipangilio mbalimbali kwaajili ya App hii, unachotakiwa kufanya ni Kuchagua Number of Picture, hii ikiwa na maana idadi ya picha zitazochuliwa na App hiyo pale mtu atakapo shika simu yako, unaweza kubadilisha na kuweka picha mbili kulingana na pendekezo lako.
MUHIMU
Sehemu hiyo utaona sehemu nyingine iliyo andikwa Detection Behavior, ni muhimu kwani inasaidia kuweza kuseti app hii iweze kupiga picha baada ya kitendo gani, yaani pale mtu atakapo washa kioo cha simu yako au pale mtu atakapo kosea password kwenye simu yako.
9. Chagua sehemu ya Always kama unataka picha ichukuliwe pale kioo kinapowashwa yani kwa mfano unapokuwa umeweka simu yako chini, na pia unaweza kuchagua Fail pale mtu anapokosea kuweka password kwenye simu yako.
kwa kufanya hatua hizi basi utakuwa umeweka ulinzi kwenye simu yako na kila mara utakapo kuwa umeweka mahali simu yako pale mtu atakapo ishika basi mtu huyo ataweza kupigwa picha moja kwa moja bila yeye kujua na utaweza kuikuta picha hiyo ndani ya App hiyo pale tu unapo ifungua. Na kama simu yako imeibiwa basi picha ya mtu huyo aliye iba unaweza kuikuta kwenye tovuti au App ya Google Photo ambayo inakuwa kwenye kila akaunti ya Gmail.
Mpaka Hapo Utakuwa Umefanikisha kujua mtu mtu anaposhika simu yako bila wewe kujua. Kwa wale wenye wapenzi wenye wivu kupitiliza nadhani hii itakufaa sana pale unapokuwa umelala alafu mtu anashika simu yako bila hata wewe kujua. Natumaini maujanja haya yatakusaidia kwa namna moja au nyingine. Kumbuka Kudownload Application Yetu Hapo Chini
0 Comments