Kipindi
cha nyuma nilishawahi kupata maoni ili niweze kusaidia kampuni moja
changa ambayo ilikuwa inataka kuwezesha huduma ya WiFi kwenye eneo
fulani hapa Tanzania, Lakini baada ya muda kidogo nilipata tena maoni
niweze kusaidia kampuni hiyo jinsi ya kutambua password za Wifi ambazo
zilikuwa zimewekwa kwa bahati mbaya na mfanyakazi wa zamani wa sehemu
hiyo.
Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo nilitumia kuweza kupata
password ya WiFi hiyo na labda pengine na wewe maujanja haya yanaweza
kukusaidia kupata password ya kifaa chako cha WiFi ambacho umeisahau
password yake kwa namna moja ama nyingine.
KUMBUKA : Njia hii ni
kwaajili ya elimu hivyo hakikisha hutumii njia hii vibaya kwa namna
yoyote ile, Kumbuka nia ni kuelimishana na kusaidiana kwenye matatizo ya
kiteknolojia yanayotokea kila siku na sio vinginevyo. Baada ya kusema
hayo basi twende tukangalie njia hii. Kwa Kutumia App ya Wifi Wps Wpa Tester
Kama
kwa namna yoyote ile umesahau password yako ya WiFi, kwa kutumia app
ya Wifi Wps Wpa Tester utaweza kupata password yako. Njia hii inahusisha
simu ya Android na ni moja kati ya njia rahisi kwenye list hii.
Unachotakiwa kufanya ni kudownload app ya Wifi Wps Wpa Tester kwa
kubofya hapo chini, kisha endelea kufuata maelekezo zaidi hapo chini.
Pia kama simu umeroot simu yako basi njia hii ni rahisi zaidi.
Baada
ya kudownload App hii washa app hii kisha bofya kitufe cha duara upande
wa kushoto juu kisha utaona inatafuta WiFi zote zilizopo karibu na
wewe, kumbuka kuwasha router yako au kifaa chako cha WiFi ambacho
umesahau password.
Baada
ya kutafuta na kuona jina la WiFi yako, angalia kwa pembeni kwenye jina
la WiFi yako kwenye app hiyo kama jina la WiFi yako lina kufuli la rangi ya kijani kwa pembeni basi unaweza kupata password ya WiFi hiyo.
Lakini pia kama mbele ya jina la WiFi yako kuna kufuli la rangi nyekundu
basi pengine ni vyema kujaribu njia ya pili kwenye makala hii. Kama
kufuli mbele ya jina la WiFi yako ni rangi ya kijani basi endelea kwa
kubofya hapo kisha chagua njia moja kati ya zilizo owanishwa, kumbuka
kupata jina la Wifi yako inaweza kuchukua muda kutokana na ugumu wa
password yako. Pia kama simu yako iko rooted basi kazi hii inachukua
muda mfupi zaidi.
Kwa kutumia App ya ES File Explorer (Simu zilizoko Rooted)
Kwa
wale ambao wame root simu zao basi unaweza kufuata njia hii ambayo mimi
ndio iliyo nisaidia zaidi kwa kuwa nilikuwa na simu ambayo iko rooted.
Njia hii ni rahisi lakini haitofanya kazi kwenye simu ambazo haziko
rooted. Kama unataka kujifunza kuroot simu unaweza kusoma makala jinsi ya kuroot simu bila kutumia kompyua na pia jinsi ya kuroot simu yoyote ya tecno. Kumbuka kuwa makini wakati unaroot simu yakokwani unaweza kuharibu simu yako.
Kwa
kuanza kama tayari umesha root simu yako unatakiwa kupakua app ya ES
File Explorer kupitia link hiyo hapo chini. Baada ya kudownload endelea
kufuata hatua hapo chini.
Baada
ya kudownload App ya ES File Explorer fungua App hiyo kisha bofya Menu
iliyoko upande wa kushoto kisha chagua Root Explorer.
Baada
ya kuwasha sehemu hiyo, utaweza kuangalia file za ndani kabisa za simu
yako hivyo kuwa makini usije kufuta kitu muhimu kwenye simu yako. Sasa
peruzi kwenye file lililo andikwa “Data” kufungua file hilo kisha endelea kwenye hatua inayofuata.
Baada ya kufungua folder la Data ndani yeke utakutana na folder lingine linaloitwa “Misc“, fungua folder hilo kisha endelea kwenye hatua inayofuata.
Ndani ya folder la Misc unatakiwa kutafuta Folder lililo andikwa WiFi na ndani ya hilo folder kuna file lililo andikwa ‘wpa_supplicant.conf’ fungua file hilo ambalo utakuta lipo kwenye mfumo wa XML na kisha fuata hatua zinazofuata.
Sasa baada ya kufungua file hilo fafuta maneno SSID na pia tafuta PSK,SSID
ni jina la WiFi yenyewe na PSK hiyo ndio password ya WiFi yenyewe. Copy
file password hizo kisha weka kwenye WiFi yako na utaona tayari
umeunganishwa na WiFi. Kumbuka wakati unafanya yote haya WiFi ya kifaa
husika inatakiwa kuwa imewashwa.
Pia kumbuka ili kuweza kufanya hatua hizi unahitaji App hii ya pro hivyo app hiyo unaweza kuipata kwa kutumia link hapo chini.
Na
kwa kupitia njia hizi natumaini unaweza kupata password ya WiFi yako.
Kumbuka tafadhali usitumie njia hii vibaya kwani nauhakika utapata tabu
sanaaa.
0 Comments