Hivi karibuni WhatsApp imekuwa ikifanya majaribio ya sehemu mpya
ambazo zinasemekana zinakuja kubadilisha kabisa muonekano wa programu
hiyo pamoja na jinsi programu hiyo inavyofanya kazi.
Moja ya sehemu hizi ni pamoja na sehemu mpya ambayo itakuwezesha kufunga programu hiyo kwa kutumia sehemu ya Fingerprint
kwa simu zenye uwezo huo. Sehemu hii inamuwezesha mtumiaji kufunga
programu yake ya WhatsApp kabisa hadi pale atakapoweka alama yake ya
kidole ndipo aweze kuingia kwenye programu hiyo.
Lakini pia ripoti kutoka tovuti ya WABetaInfo
zinadai kuwa, sehemu hiyo ya kufungua programu hiyo kwa kutumia alama
za vidole itakuja sambamba na sehemu nyingine ambayo pengine watumiaji
wengi wanaweza wasi ipende sana. Inasemekana kuwa pale mtumiaji anapo
washa sehemu hii kupitia programu ya WhatsApp basi moja kwa moja atakuwa
amewasha sehemu nyingine ambayo itakuwa ina mzuia mtumiaji kuchukua
screenshot kwenye chat zake ndani ya programu hiyo.
Kifupi
ni kuwa pale utakapo washa sehemu ya Fingerprint kwenye programu ya
WhatsApp hutoweza kuchukua picha za screenshot ndani ya programu hiyo
hadi hapo utakapo zima sehemu hiyo. Hata hivyo inasemekana pia baada ya
kuwasha sehemu hiyo utaweza kujibu meseji kupitia sehemu ya Notification
juu ya simu yako.
Kwa sasa bado hakuna taarifa za chazo cha
WhatsApp kuweka sehemu hii ya kuzuia mtumiaji binafsi kuchukua picha za
screenshot za chat zake mwenyewe na pia bado hakuna taarifa lini sehemu
hii itakuja kwenye programu za WhatsApp. Hata hivyo sehemu ya kufunga
programu hiyo kwa kutumia alama za vidole tayari inapatikana kwenye simu za mfumo ya iOS.
Binafsi
sioni haja ya sehemu ya kujizuia mwenyewe kuchukua screenshot ya chat
zako mwenyewe hivyo sioni kama kuna maana ya sehemu hii kuwepo sambamba
na sehemu ya muhimu kama ya kufungua programu hiyo kwa kutumia alama za
vidole, Vipi kwako unaonaje kuhusu ujio wa sehemu hii..? tuambie mawazo
yako kwenye sehemu ya maoni hapo chini.
0 Comments