Kupitia makala hii nitaenda kukujulisha njia rahisi ambazo unaweza kuzitumia kuwasha sehemu ya muonekano wa giza kwenye kompyuta zenye mifumo ya Windows 10 pamoja na MacOS. Njia hizi ni rahisi sana na zinahitaji kompyuta zote ziwe na mfumo mpya wa uendeshaji, kama unatumia Windows unatakiwa kuwa na mfumo wa Windows 1809. Pia kama unatumia mfumo wa MacOS basi hakikisha kompyuta yako inayo mfumo mpya wa macOS Mojave.
Kama tayari kompyuta yako inayo mifumo yote hiyo basi unaweza kuendelea kwenye hatua za kuwasha muonekano mweusi au Dark Mode kwenye kompyuta yako.
YALIYOMO
- Jinsi ya Kuwasha Dark Mode Kwenye Windows
- Jinsi ya Kuwasha Dark Mode Kwenye macOS
Jinsi ya Kuwasha Dark Mode Kwenye Windows
Kama unavyoweza kuona kwenye video hapo juu hatua hizi ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye sehemu ya bendera ya Windows iliyopo chini upande wa kushoto, kisha bofya hapo alafu bofya sehemu ya Settings ambayo nayo ipo upande wa kushoto pembeni.
Baada ya hapo utaona ukurasa wa Settings umefungua kisha bofya sehemu ya personalization, baada ya hapo kwenye ukurasa una fuata bofya sehemu ya Colors iliyopo pembeni upande wa kushoto juu baada ya hapo kwenye ukurasa unafuatia shuka mpaka chini mwisho kabisa utaona sehemu iliyo andikwa choose a defult mode kisha chagua Dark na hapo utakuwa umemaliza.
Kumbuka kama unao mfumo wa zamani wa Windows 10 utaweza kupata muonekano mweusi kwenye apps mbalimbali za windows na sio kwenye File Explorer.
Jinsi ya Kuwasha Dark Mode Kwenye macOS
Kwa upande wa macOS pia ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kubofya sehemu ya sehemu ya System preference sehemu hii inapatikana kwenye menu bar iliyopo chini au kwa kupitia sehemu ya About iliyopo kwenye alama ya Apple iliyopo juu upande wa kushoto. Baada ya hapo chagua General baada ya hapo chagua Dark sehemu ambayo ipo upande wa kulia juu kwenye ukurasa ulifunguka, Baada ya hapo utakuwa umemaliza.
Njia hizi ni za muhimu sana kwako hasa kama unatumia kompyuta wa muda mrefu kwani hii itakusaidia kulinda macho yako. Kama unataka kujua zaidi kuhusu njia nyingine za kulinda macho yako soma hapa kuhusu sheria ya 20 20 20 ambayo ni muhimu kwa watumiaji wa kompyuta.
0 Comments